MAJALIWA: MRADI WA SGR UTAKAMILIKA KAMA ULIVYOPANGWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) na kwamba Serikali itaendelea kuhakikisha mradi huo unajengwa kwa viwango na kukamilika kama ilivyobainishwa kwenye mkataba. Amesema kuwa ujenzi wa reli hiyo unaendelea vizuri katika vipande vyote na kwamba Serikali itahakikisha mradi huo haukwami na itakabiliana na viashiria